Klabu ya Stade Malien yaweka historia CAF
9 Februari 2026
Michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika imeendelea kutimua vumbi katika viwanja mbalimbali usiku wa kuamkia leo. Klabu ya soka ya Stade Malien ya nchini Mali imekuwa klabu ya kwanza katika nchi hiyo kufikia hatua ya mtoano ya Ligi ya Mabingwa ya CAF baada ya kuifunga Esperance ya Tunisia bao 1-0 mjini Bamako.
Matokeo hayo yameifanya Stade Malien kuwa kileleni mwa kundi D na alama 11,Esperance na Petro Luanda ya Angola wakiwa na alama sita huko Simba ya Tanzania ikiwa mkiani na alama mbili pekee..
Pyramids ya Misri ambao ni mabingwa watetezi wa michuano hiyo walitoka nyuma dhidi ya Rivers United ya Nigeria na kushinda 4-1.
Saint-Eloi Lupopo kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini zilitoka sare ya 1-1 mjini Lubumbashi.