1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Migogoro

Kitisho cha waasi wa M23 chazidi kuukabili mji wa Goma

19 Februari 2024

Hali ya usalama inaendelea kuzorota katika mji wa Goma, mkoani Kivu Kaskazini, kutokana na tishio la waasi wa M23 linaloukabili mji huo Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

https://p.dw.com/p/4cZIP
DR Kongo Bunagana Truppen der EAC
Picha: Alain Uaykani/Xinhua/picture alliance

Baadhi ya wakaazi wa Goma wameanza hata kuondoka kwenye mji huo, licha ya juhudi za nchi za eneo hilo kutafuta suluhisho la mgogoro kati ya Kongo na Rwanda ambayo inatuhumiwa kuwaunga mkono M23. 

Tangu mabomu yanayovurumishwa kutoka kwenye maeneo ya waasi yaanze kufika Goma, baadhi ya wakaazi wanakimbilia miji mingine, wakiwa na hofu kuhusu usalama wao.

Jean de Dieu KULONDWA, mkaazi wa Himbi, sasa yupo peke yake nyumbani kwake, baada ya wanafamilia wote kuhamia Bukavu mwishoni mwa wiki kutokana na kuzorota hali ya usalama.

Soma pia:Bomu laupiga uwanja wa ndege wa Goma, mashariki mwa Kongo

"Wakati mabomu yalipoanguka pia kwenye uwanja wa ndege, ndipo familia nzima ilipoogopa hadi kuamua kuondoka mjini." Alisema na kuongeza ku Kwa sasa, amebakia peke yake nyumbani, lakini hali ya usalama bado inatia mashaka.

Asubuhi ya Jumamosi tarehe 17 Februari, mabomu mawili yaliripuka katika uwanja wa ndege wa Goma, yakisababisha uharibifu wa ndege za raia kulingana na jeshi la Kongo, ambalo lilizungumzia mashambulizi yaliyofanywa na ndege zisizo na rubani za jeshi la Rwanda.

Mkutano mdogo Adis Ababa una matokeo gani?

Viongozi wa nchi za eneo hilo, ikiwa ni pamoja na Felix Tshisekedi wa Kongo na Paul Kagame wa Kagame, wamekutana Addis Ababa kwa mkutano mdogo kuhusu mgogoro wa Mashariki mwa Kongo.

Rais wa Rwanda Paul Kagame kushoto, wa Angola Joao Lourenco katikati na Felix Tshisekedi wa DR Kongo
Rais wa Rwanda Paul Kagame kushoto, wa Angola Joao Lourenco katikati na Felix Tshisekedi wa DR KongoPicha: JORGE NSIMBA/AFP

Lakini kulingana na mchambuzi wa maswala ya kijamii na kisiasa, Johnson Butaragaza, jambo pekee zuri kwa mkutano huo lilikuwa kuthibitisha mbele ya dunia uhusika wa moja kwa moja wa Rwanda katika mgogoro ambao mara zote imekanusha kuhusika kwake: 

 "Nadhani mkutano huo ulikuwa ni kuthibitisha mbele ya dunia kwamba kinachoendelea Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, ni shambulio la moja kwa moja kutoka Rwanda."

Aliongezea hoja yake kwa kusema kwamba "Kwa sababu kama siyo Rwanda, Umoja wa Afrika usingeliitaka Kongo kuzungumza na Rwanda, bali badala yake na M23." 

Soma pia:Marekani inalaani ghasia mashariki mwa DR Kongo

 Mkutano huu ulioitishwa na Rais wa Angola, uliangazia umuhimu wa kurudi kwenye mazungumzo yenye kujenga na kurejesha uhusiano kati ya Kongo na Rwanda, lakini kwa Butaragaza, inahitaji zaidi ya hili kuleta amani Kongo, hasa ikizingatiwa kwamba Rais Tshisekedi hajabadili uamuzi wake wa kutokufanya mazungumzo yoyote mpaka pale jeshi la Rwanda litakapoondoka kwenye ardhi yake:

"Kwa maneno mengine, hii inamaanisha, kama hamtaondoka, hatuzungumzi na tutaendelea na vita." Mchambuzi huyo alifasili kauli na  msimamo wa Rais wa Kongo Felix Tshisekedi.

"Umoja wa Afrika unapaswa kujitokeza kama taasisi inayofanya kazi kwa umoja na maelewano ya nchi za Afrika, na hapa tuna nchi inayoshambulia uhuru wa nchi nyingine, hivyo hatua zinazofaa zinapaswa kuchukuliwa."  Aliiambia DW

Kwenye hafla hiyo hiyo ya Mkutano wa 37 wa kawaida wa Umoja wa Afrika, marais NDAYISHIMIYE wa Burundi, Cyril Ramaphosa wa Afrika Kusini na Tshisekedi wa Kongo, walifanya mkutano wa pande tatu kuhusu kupeleka wanajeshi wa Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika, SADC, mashariki mwa Kongo.

Maelfu wakimbia vita Sake