1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Migogoro

Angola yaongoza mkutano wa kufufua juhudi za amani DRC

Sylvia Mwehozi
17 Februari 2024

Rais wa Angola Joao Lourenco ameongoza mkutano mdogo mjini Addis Ababa, katika juhudi za kufufua mazungumzo ya amani katika eneo lililokumbwa na ghasia mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

https://p.dw.com/p/4cVkL
Joao Lourenco
Rais wa Angola Joao Lourenco Picha: Amanuel Sileshi/AFP/Getty Images

Rais wa Angola Joao Lourenco ameongoza mkutano mdogo mjini Addis Ababa, katika juhudi za kufufua mazungumzo ya amani katika eneo lililokumbwa na ghasia mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

Mkutano huo, uliofanyika katika mkesha wa mkutano wa kilele wa Umoja wa Afrika, unafuatia kuongezeka kwa mapigano katika eneo la mashariki.

Miongoni mwa yaliyojadiliwa ni kurejea katika mazungumzo kati ya Kongo na Rwanda, kusitishwa mara moja kwa mapigano na kuondoka kwa waasi wa M23 kutoka maeneo wanayoyadhibiti.

Juhudi za kidiplomasia hadi sasa zimeshindwa kuzima mzozo kati ya kundi la waasi la M23 na jeshi la Kongo katika eneo lenye utajiri mkubwa wa madini mashariki mwa taifa hilo kubwa la Afrika ya kati.