Kipigo kingine kwa rais George Walker Bush | Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili | DW | 28.08.2007
 1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages

Timu Yetu

Kipigo kingine kwa rais George Walker Bush

Mwanasheria mkuu wa Marekani Alberto Gonzales mshirika wa karibu wa rais Bush ajiuzulu

Alberto Gonzales

Alberto Gonzales

Gonzales alijiuzulu jana baada ya kipindi kigumu cha kukosolewa na wapinzani wake kutoka vyama vya Republican na Demokratic.

Gonzales mshirika mkubwa wa rais Bush ametangaza kwamba atajiuzulu kuanzia tarehe 17 mwezi ujao.Kazi yake Gonzales imekuwa ikitiliwa shaka na wapinzani wake hasa baada ya kutokea kashfa ya kuwafuta kazi waongozaji mashtaka wanane wa serikali hatua ambayo ilitajwa na wengi kuwa ilichochewa kisiasa.

Akizungumzia kujiuzulu kwa mwanasheria huyo rais Bush alisema,

‘’ inasikitisha kwamba katika wakati kama huu mtu mwenye kipaji na wakutegemewa kama Gonzales anazuiwa kufanya kazi muhimu kutokana na kupakwa matope jina lake kwa sababu za kisiasa.’’

Chama cha Demokratic kimeapa kuendelea kufanya uchunguzi kuona ikiwa Gonzales alishirikiana na ikulu katika kuwafurusha kazini waendesha mashtaka 8 waserikali kwa sababu za kisiasa.

 • Tarehe 28.08.2007
 • Mwandishi Saumu Mwasimba
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/CB1g
 • Tarehe 28.08.2007
 • Mwandishi Saumu Mwasimba
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/CB1g
Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com