Papa Leo XIV kuanza ziara barani Afrika wiki ijayo
9 Aprili 2026
Matangazo
Lengo la ziara hiyo ni kuwashawishi viongozi wa dunia kuyashughulikia masuala muhimu ya bara hilo ambapo kuna idadi kubwa ya Wakatoliki.
Mataifa atakayotembelea Papa Leo kwenye ziara hiyo ni Algeria, Cameroon, Angola na Guinea ya Ikweta. Kiongozi huyo wa Kanisa Katoliki duniani atakuwa Papa wa Kwanza kuizuru Algeria, taifa lenye Waislamu wengi lenye takriban watu milioni 48 na Wakatoliki wasiozidi 10,000.
Mazungumzo na viongozi, wazawa yatazamiwa
Kwenye ziara hiyo itakayohusisha miji 11, atakutana na viongozi na kuzungumza na wazawa ambapo anatarajiwa kuhamasisha amani, majadiliano na kutoa ujumbe wa matumaini. Papa Leo XIV, anatazamiwa pia kutembelea maeneo ya kihistoria na yale yaliyoathiriwa na migogoro na majanga.