Kenya yatambulisha kikosi cha Olimpiki Tokyo | Michezo | DW | 21.06.2021
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Michezo

Kenya yatambulisha kikosi cha Olimpiki Tokyo

Kenya imekitambulisha kikosi chake kitakachoshiriki katika Michezo ya Olimpiki ya Tokyo kikiwa na orodha ya Zaidi ya wanariadha 40 wakiwemo. Wanariadha Timothy Cheruiyot na Conseslus Kipruto hawakufuzu

Kenya imekitambulisha kikosi chake kitakachoshiriki katika Michezo ya Olimpiki ya Tokyo kikiwa na orodha ya Zaidi ya wanariadha 40 wakiwemo bingwa wa dunia Hellen Obiri na mshindi wa dhahabu katika Olimpiki ambaye ni bingwa mtetezi wa mbio za mita 1,500 Faith Chepngetich.

Majina maarufu yaliyoachwa nje ni bingwa wa ulimwengu wa mita 1,500 kwa wanaume Timothy Cheruiyot na bingwa mtetezi wa Olimpiki katika mbio za mita 3,000 kuruka viunzi na maji Conseslus Kipruto baada ya wote kushindwa katika mbio za mchujo.

Timu hiyo pia inawajumuisha wanariadha Eliu Kipchoge, Brigid Kosgei na Geoffrey Kamworor ambaye atashiriki mbio za mita 10,000. TeamKenya inapanga kelekea Japan Julai 5 kwa ajili ya kuweka kambi mjini Kurume kwa ajili ya Michezo hiyo itakayoanza Julai 23.

AP/Reuters