Kenya yamteua Balozi Amina Mohamed WTO | Matukio ya Afrika | DW | 16.01.2013
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Matukio ya Afrika

Kenya yamteua Balozi Amina Mohamed WTO

Serikali ya Kenya imemteua Balozi Amina Mohamed kuwania nafasi ya Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Biashara Duniani (WTO).

WIKIPEDIA Die Welthandelsorganisation (englisch World Trade Organization, WTO; französisch Organisation mondiale du commerce, OMC; spanisch Organización Mundial de Comercio, OMC) ist eine internationale Organisation mit Sitz in Genf, die sich mit der Regelung von Handels- und Wirtschaftsbeziehungen beschäftigt. Sie wurde am 15. April 1994 aus dem General Agreement on Tariffs and Trade (GATT) in der Uruguay-Runde nach siebenjähriger Verhandlungszeit gegründet. Am 1. Januar 1995 nahm sie ihre Arbeit in Genf auf. Die WTO ist neben dem IWF und der Weltbank eine der zentralen internationalen Organisationen, die Handels- und Wirtschaftspolitik mit globaler Reichweite verhandelt.

Logo Welthandelsorganisation

Balozi Amina ambaye anahudumu katika wadhifa wa Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa na vile vile Naibu Mkurugenzi wa Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa (UNEP) lililo na makao yake makuu mjini Nairobi alizindua kampeni yake jana jioni katika hoteli ya Intercontinental.

Hafla hiyo ilihudhuriwa na Waziri wa Mambo ya Kigeni wa Kenya, Prof. Sam Ongeri, Waziri wa Biashara, Moses Wetangula, na maafisa wa kibalozi kutoka nchi mbali mbali za ulimwengu.

Balozi Amina ambaye kitaaluma ni wakili, amewahi kufanya kazi katika serikali ya Kenya akiwa mshauri wa kisheria katika wizara ya mambo ya nje. Amewahi kuwa Balozi wa Kenya katika Umoja wa Mataifa na amekuwa mwanachama wa bodi kuu na kamati za mashirika mbali mbali ya Umoja wa Mataifa.

Balozi Amina Mohammed ataaanza kampeni yake kwa kutembelea miji mikuu ya mataifa wanachama wa Shirika la WTO, ambayo itakampeleka hadi Geneva tarehe 30 mwezi huu ambapo atakutana na wagombea wenzake wanane wanaopigania nafasi hiyo.

Wagombea wengine wanaopigania nafasi hiyo ni; Alan John Kwadwo kutoka Ghana, Bi Anabel González wa Costa Rica, Bi Mari Elka Pangestu kutoka Indonesia, Tim Groser kutoka New Zealand, Ahmad Thougan Hindawi kutoka nchini Jordan, Herminio Blanco kutoka Mexico, Bwana Taeho Bark kutoka Jamuhuri ya Korea Na Roberto Carvalho de Azevêdo kutoka Brazil.

Amina anasema endapo atachaguliwa lengo lake kuu litakuwa kukabiliana na changamoto zinazokumba shirika la WTO ikiwa ni pamoja na mashauri ya kibiashara katika uchumi wa dunia.

Mwandishi: Alfred Kiti/DW Nairobi
Mhariri: Josephat Charo