1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kenya: Polisi yatawanya maandamano ya upinzani

Grace Kabogo
20 Machi 2023

Polisi wa kutuliza ghasia nchini Kenya leo wametumia mabomu ya kutoa machozi na maji ya kuwasha dhidi ya msafara wa kiongozi wa upinzani Raila Odinga.

https://p.dw.com/p/4Owqz
Kenia l Proteste in Nairobi l Ausschreitungen mit der Polizei
Picha: Brian Inganga/AP/picture alliance

Hayo yanajiri wakati ambapo makabiliano yakipambana moto katika maandamano ya kupinga kupanda kwa gharama ya maisha. Polisi waliutawanya msafara wa magari wa Odinga, ambaye ameitisha maandamano ya nchi nzima kuipinga serikali ya William Ruto kutokana na mfumuko wa bei na madai ya wizi katika uchaguzi wa mwaka uliopita.

Soma pia: Maandamano yashuhudiwa Kenya na Afrika Kusini

Odinga, aliyesisitiza kuwa maandamano hayo yataendelea licha ya kutopewa kibali cha polisi, alitarajiwa kuzungumza na waandishi habari katika hoteli moja mjini Nairobi, lakini alilazimika kuondoka. Watu kadhaa wamekamatwa, wakiwemo wabunge wawili wa upinzani na kiongozi wa wachache katika Baraza la Seneti, Stewart Madzayo.

Makamu wa Rais, Rigathi Gachagua ametoa wito wa kusitisha maandamano hayo, akisema yameisababishia Kenya hasara ya shilingi bilioni mbili za Kenya.