Kanisa la Kiinjili latoa tahadhari za kisiasa | Matukio ya Kisiasa | DW | 29.05.2017
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Berlin

Kanisa la Kiinjili latoa tahadhari za kisiasa

Joto, matukio, na Ulinganifu: ndio wimbo wa amani wa Kongamano la Kanisa la Kiinjili lililomalizika. Limetoa ishara za karipio zinazohitajika zaidi dhidi ya wanasiasa, anasema Astrid Prange katika maoni yake

Siasa?  Hapana! Ni Ujumbe wa Kanisa la Kiinjili baada ya kumalizika kongamano la Berlin na Wittenberg: katika ujumbe wake kanisa la Kiinjili linasema, Jihadharini na matamshi ya kufuata upepo, wala msishabikie matamshi ya wanasiasa wanaotafuta umaarufu kwa kutumia hoja za kijuu juu na siasa zenye mtazamo mkali na pia mjihadhari na kuingia hatiani kwa kuitumia vibaya siasa kwa kisingizio cha dini.

Kwa nini? Kwa sababu watu hao si wanasiasa, hawahusiani na uchumi, na wala sio Waislamu au Wakristo. Kongamano la Kanisa la Kiinjili linachangia katika kupunguza uadui, kuwakutanisha watu na kuleta uwezekano wa kuendesha mijadala ya haki.

Hata kama matukio 2,500 yana utata kutokana na tofauti zake na Uprotestanti, matukio hayo yatakuwa yanasababisha matatizo mengi kwa washirika na waumini wake. Imebainika hazina ambayo bado ipo katika siasa za Ujerumani ambayo ni nia na maadili katika mtazamo wa Kikristo unaozingatia ubinadamu kwa wanawake na wanaume, ambao huunganisha mamlaka yao ya kisiasa na maadili haya.

Utambulisho badala ya kushuka Thamani

Hii ni kutokana kuongezeka kwa idadi ya wanasiasa ambao hujenga wasifu wao kwa kutumia kushuka thamani ya wengine, wizi wa kura wa aina hii haupaswi kupuuzwa. Ni rais wa Marekani Donald Trump tu ndiye aliyeonyesha jinsi muundo huu unavyofanya kazi. Jamii ya Ulaya yenye sifa ya thamani sasa inashangaza kutokana na takwimu za chuki dhidi ya Umoja wa Ulaya, lakini wakati huo huo wanafaidika kwa kupata fedha nzuri kutoka kwenye makao hayo makuu mjini Brussels.

Die Reformationsbotschafterin Margot Kaessmann hielt am Samstag 27 05 2017 beim Kirchentag auf dem Bibelarbeit (Imago)

Baadhi ya wageni waliohudhuria kongamano la Kanisa la Kiinjili 2017

Kwa hiyo wanasiasa wanaowalaani waliochaguliwa ndio hao hao tena wanaokunywa maji kutoka kwenye mto wa wanasiasa wanaotumia hoja za chuki, kwa maneno mengine wanafaidika kwa matamshi ya wanasiasa hao.  Kongamano hilo la Kanisa la Kiinjili linaonyesha kuwa mambo ni tofauti. Katika wadhfa wake wa urais, wapo wawakilishi wanaowajumisha wanasiasa na wanauchumi ambao wanatafuta maslahi tofauti, ijapokuwa maadili ndio jambo moja linalowaunganisha, kati ya wawakilishi hao ni pamoja na Waziri wa mambo ya  Ndani wa Ujerumani Thomas de Maiziere (CDU), Mbunge Sven Giegold wa chama cha Kijani na Mfamasia Andreas Barner.

Mkusanyiko wa Thamani

Pamoja na tofauti zilizopo, Kongamano hilo la Kanisa la Kiinjili limeonyesha kuwa hadi sasa ipo sehemu kubwa kutoka kwenye tabaka la wanasiasa nchini Ujerumani. Kongamano hilo lilifaulu kuwakutanisha viongozi wa kiroho wa dunia pamoja na wanasiasa mashuhuri mjini Berlin katika mkutano wa siku tano ikiwa ni pamoja na Sheikh mwenye mamlaka ya juu wa madhehebu ya Sunni, Sheikh Ahmad al-Tayyeb kutoka Misri, vilevile alikuwepo Thabo Makgoba, waziri mkuu wa  wa Kanisa la Anglikana nchini Afrika Kusini, mwenyekiti wa Kongamano la Maaskofu wa Ujerumani Kadinali Reinhard Marx, na bila shaka rais wa zamani wa Marekani Barack Obama, aliye wavutia wengi katika mkutano huo.

Bila shaka, Kongamano la Kanisa la Kiinjili linauona ugumu wa kutekeleza mambo katika enzi hii ya Donald Trump. Itakavyokuwa lakini mawazo yake (Trump) yana nguvu zaidi kuliko habari mbaya za kila siku kutoka ikulu ya Marekani.

Bila matumaini haya hakutakuwa na kongamano la Kanisa la Kiinjili, hakutakuwa na Uprotestanti, hakutakuwa na imani, na hakutakuwa na Mageuzi. Historia ya miaka 500 ya matengenezo ya Kanisa, ambayo haina dalili ya kumalizika hivi karibuni, inavuta bado pumzi ndefu. Hatua kama hizi japo za polepole zitasaidia kujenga matumaini ya kupata matokeo bora.

Mwandishi: Zainab Aziz/ Prange, Astrid/DW LINK: http://www.dw.com/a-39016446

Mhariri. Mohammed Abdul-Rahman

Matangazo

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com