1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Jeraha la goti hundea likamuweka nje kwa muda Emre Can

1 Machi 2026

Nahodha wa kikosi cha Borussia Dortmund Emre Can huenda akakosekana kwa muda mrefu uwanjani baada ya kuumia goti vibaya katika mechi ya Bundesliga dhidi ya Bayern Munich, ambayo Bayern iliibuka na ushindi wa 3–2.

https://p.dw.com/p/59cYl
Dortmund 2026 | Bundesliga: Borussia Dortmund vs. FC Bayern München – Emre Can
Emre Can akitoka nje ya uwanja baada kupata jeraha la godi katika mechi dhidhi ya Bayern Munich.Picha: Federico Gambarini/dpa/picture alliance

Ingawa taarifa rasmi bado haijatolewa, kocha Niko Kovač amesema dalili zinaonyesha jeraha la mshipa wa goti ambalo litakuwa pigo kubwa kwa timu.

Can alipata jeraha hilo mwishoni mwa kipindi cha kwanza, alikataa kutoka nje na akarudi uwanjani kwa muda mfupi, lakini hakuweza kutembea vizuri na hatimaye akaanguka chini na kulazimika kutoka akichechemea. Kovač amesema madaktari hawakumzuia kuendelea kwa sababu mchezaji mwenyewe alisisitiza kubaki uwanjani.

Iwapo vipimo vitathibitisha jeraha hilo msimu wa Can unaweza kuisha mapema, na pia atakosa kushiriki Kombe la Dunia la majira ya joto. Can, ambaye ni mchezaji wa timu ya taifa ya Ujerumani, amekuwa mhimili muhimu Dortmund na kiongozi ndani ya uwanja.