JEDDAH: Rais Abbas azuru Saudi Arabia
12 Septemba 2007Matangazo
Rais wa mamlaka ya Palestina, Mahmoud Abbas, amesema amezungumza na mfalme wa Saudi Arabia juu ya mkutano wa kimataifa kuhusu amani ya mashariki ya kati na hali ya kisiasa katika maeneo ya Wapalestina.
Rais Abbas amefutilia mbali uwezekano wa kufanya mazungumzo na kundi la Hamas mpaka litakapourejesha ukanda wa Gaza katika utawala wa mamlaka ya Palestina.
Rais Abbas ambaye ameondoka mjini Jedda kuelekea Amman Jordan, amesema atakutana na mfalme Abdullah II wa Jordan hii leo.