1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Italia yatuma mawaziri Afrika kupata mikataba ya nishati

Amina Mjahid
20 Aprili 2022

Serikali ya Italia imewatuma mawaziri wake wawili barani Afrika kwa ziara ya kutafuta mikataba mipya ya nishati katika wakati Italia inahangaika kujinasua na matumizi ya gesi kutoka Urusi kutokana na vita nchini Ukraine.

https://p.dw.com/p/4A8dy
Italien |  Mario Draghi
Picha: ALBERTO PIZZOLI/AFP

Waziri Mkuu wa Italia Mario Draghi analenga kuyatumia mataifa mawili ya Angola na Jamhuri ya Congo kama wasambazaji mbadala wa nishati ya Urusi inayofikia asilimia 45 ya gesi yote inayotumika nchini  Italia.

Serikali ya Draghi imewatuma waziri wa mambo ya kigeni, Luigi Di Maio, na mwenzake wa Ikolojia, Roberto Cingolani, kwenda mjini Luanda leo Jumatano na baadaye mjini Brazzaville kujadili uwezekano wa kununua nishati kutoka Angola na Jamhuri ya Congo.

Italia, ambayo imeapa kumaliza utegemezi wa nishati ya Urusi, tayari imetia saini mikataba ya kununua gesi kutoka Algeria na Misri na inapanga pia kufanya mazungumzo ya kununua gesi nchini Msumbuji mnamo mwezi Mei.

chanzo: ap