1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaIsrael

Israel yashambulia Gaza na maeneo ya kusini mwa Lebanon

7 Aprili 2023

Jeshi la Ulinzi la Israel limesema limevilenga kwa mashambulizi makali vituo vya Hamas, katika ukanda wa Gaza na kusini mwa Lebanon na kwamba hawataruhusu kundi hilo la kigaidi kuendesha shughuli zake nchini humo.

https://p.dw.com/p/4Poe6
Libanon Ras al-Ain | Zerstörung nach israelischen Luftangriffen
Picha: Aziz Taher/REUTERS

Chanzo cha usalama cha Lebanon kimebaini kuwa angalau milipuko mitatu ilisikika alfajiri ya leo baada ya ndege za Israel kulenga mashamba viungani mwa kambi ya wakimbizi wa Kipalestina ya Rashidiyeh karibu na mji wa Tiro kusini mwa Lebanon.

Jana,  Israel ilisema, ilinasa na kuharibu makombora 36 yaliyorushwa kutoka Lebanon ikiwa ni moja ya mashambulizi makubwa zaidi kuwahi kushuhudiwa tangu mwaka 2006. Ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini Lebanon (UNIFIL) umetoa wito kwa pande zote kusitisha mashambulizi.