1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Israel yasema imewauwa watu wawili katika Ukanda wa Gaza

15 Februari 2026

Jeshi la Israel limesema limewaua Wapalestina wawili katika Ukanda wa Gaza. Jeshi hilo limeongeza kuwa "magaidi kadhaa wenye silaha" walitambuliwa katika upande wa Israel wa kile kinachojulikana kama mstari wa njano.

https://p.dw.com/p/58nRb
Wapalestina wakagua kituo cha polisi mjini Gaza City mnamo Januari 31, 2026
Shambulizi la Israel katika ukanda wa GazaPicha: Majdi Fathi/NurPhoto/picture alliance

Mstari huo unaashiria eneo lisilokuwa na shughuli za kijeshi ambalo wanajeshi wa Israel walijiondoa kama sehemu ya makubaliano ya kusitisha mapigano na kundi la wanamgambo la Hamas.

Pia limedai kuwa "magaidi" waliibuka kutoka kwa miundombinu ya chini ya ardhi na kujificha chini ya vifusi karibu na vikosi vya Israel, na kusababisha kile ilichokiita "tishio."

Taarifa hizo hazikuweza kuthibitishwa kwa njia huru.