1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Israel yasema imemuuwa Esmail Khatib

18 Machi 2026

Waziri wa ulinzi wa Israel amesema leo kuwa jeshi la nchi hiyo limemuua waziri anayehusika na masuala ya ujasusi wa Iran Esmail Khatib.

https://p.dw.com/p/5Ad41
Iran Teheran 2025 | Esmail Khatib
Waziri anayehusika na masuala ya ujasusi wa Iran aliyeuawa Esmail Khatib.Picha: Iranian Presidency/ZUMA/picture alliance

Mauaji ya Khatib yanafuatia mauaji ya afisa mkuu wa usalama nchini Iran Ali Larijani pamoja na mkuu wa kikosi kikosi maalum cha wapiganaji cha Basij ambacho ni tawi la jeshi la walinzi wa mapinduzi jenerali Gholam Reza Soleimani.

Israel pia imeshambulia kwa mabomu sehemu ya sekta ya gesi ya Iran katika Ghuba. Haya ni kwa mujibu wa ripoti za vyombo vya habari vya pande zote mbili za vita.

Kwa upande wake, Iran imefanya mashambulizi kueleka Israel na mataifa jirani ya Ghuba huku milipuko ikisikika katika Umoja wa Falme za Kiarabu na Qatar na udunguaji ukiripotiwa Saudi Arabia.