1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Iran yashambulia Israel na mataifa jirani ya Ghuba

18 Machi 2026

Iran imejibu mauaji ya mmoja wa viongozi wake wakuu aliyeuawa katika shambulio la anga kwa mashambulizi dhidi ya majirani zake wa Ghuba na Israel kwa kutumia baadhi ya makombora yake ya kisasa ya kukwepa ulinzi wa anga.

https://p.dw.com/p/5Aayl
Iran Isfahan 2026 | shambulizi la pamoja na Marekani na Israel
Shambulizi la Marekani na Israel katika eneo la viwanda la Isfahan nchini Iran mnamo Machi 14, 2026Picha: UGC/AFP

Mashambulizi mapya yaliripotiwa mapema leo, katika mkoa mkubwa wa mashariki wa Saudi Arabia, ambao ni makazi ya visima vyake vingi vya mafuta, Kuwait, Bahrain, Qatar na Umoja wa Falme za Kiarabu.

Nchini Iran, kinu cha nyuklia cha Bushehr kililengwa kwa kombora lakini hakukuwa na majeraha wala uharibifu. Haya ni kulingana na Shirika la Kimataifa la Nishati ya Atomiki IAEA baada ya kupokea ripoti kutoka Tehran.

Mkuu wa IAEA, Rafael Grossi, amesisitiza wito wake wa kujizuia zaidi wakati wa mzozo huo ili kuzuia hatari ya ajali ya nyuklia.