1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Israel na umiliki wa kipande cha ardhi Ukingo wa Magharibi

22 Machi 2024

Waziri wa fedha wa Israel Bezalel Smotrich leo ametangaza kuwa hekta 800 za ardhi katika eneo linalokaliwa na nchi hiyo kimabavu la Ukingo wa Magharibi ni ardhi ya dola la Israel.

https://p.dw.com/p/4e268
Ukingo wa Magharibi
Ukingo wa MagharibiPicha: AHMAD GHARABLI/AFP

Waziri wa fedha wa Israel Bezalel Smotrich leo ametangaza kuwa hekta 800 za ardhi katika eneo linalokaliwa na nchi hiyo kimabavu la Ukingo wa Magharibi ni ardhi ya dola la Israel, hatua ambayo itawezesha matumizi ya ardhi hiyo kwa ujenzi wa makazi ya walowezi.

Soma: Machafuko yaongezeka Ukingo wa Magharibi

Tamko hilo la waziri wa fedha wa Israel lililotolewa katika wakati ambapo waziri wa mambo ya nje wa Marekani,Antony Blinken yuko ziarani nchini humo, linaonesha dhamira ya serikali ya Israel ya kutaka kuendelea mbele na mpango wa kujenga makaazi ya walowezi wakiyahudi katika eneo hilo la Ukingo wa Magharibi licha ya hatua hiyo kuzidi kupingwa kimataifa.

Smotrich amesema wakati kuna wale walioko nchini Israel na duniani wanaotafuta kuhujumu haki ya nchi hiyo katika maeneo ya Judea na Samaria na ndani ya Israel kwa ujumla, nchi hiyo inapigia upatu ujenzi wa makazi kupitia kufanya kazi kwa bidii na kwa hatua za kimkakati kote nchini humo. Mamlaka ya Palestina imepinga hatua hiyo.