1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Israel yaendelea kuishambulia eneo la Bureij Gaza

4 Juni 2024

Israel imeendeleza hivi leo mashambulizi yake katika Ukanda wa Gaza hasa katika eneo la kati la Bureij ambako kumeripotiwa vifo vya watu kadhaa.

https://p.dw.com/p/4gcpW
Bureij, Gaza | Jengo likiwaka moto baada ya kushambuliwa.
Jengo likiteketea kwa moto baada ya kushambuliwa na vikosi vya Israel huko katika eneo la Bureij Ukanda wa GazaPicha: Bashar Taleb/AFP/Getty Images

Jeshi la Israel limetangaza pia kuwa mateka wengine wanne waliokuwa wakishikiliwa na Hamas wameripotiwa  kufariki.

Umoja wa Mataifa umetaja wasiwasi wake kuhusu hali ya kiafya huko Khan Younis na Deir al-Balah.

Soma pia:Zaidi ya nusu ya miundombinu yote Ukanda wa Gaza imeharibiwa

Hayo yanajiri wakati Marekani imelihimiza hapo jana Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuunga mkono mpango wa awamu tatu uliotangazwa na Rais Joe Biden, ambao unalenga kumaliza vita vya takriban miezi minane huko Gaza, kuachiliwa kwa mateka na kutumwa misaada.