Serikali ya Israel imeanza kutekeleza mpango wake wa kuwaondoa maelfu ya wahamiaji kutoka Afrika walioko nchini humo, hadi ifikapo mwezi Aprili huku ikitishia kuwakamata wale watakaobaki. Hata hivyo agizo hilo limekosolewa na mashirika ya utetezi wa haki za binaadamu yakidai linakiuka haki za wahamiaji.