ISLAMABAD:Benazir Bhutto kurejea Pakistan mwezi ujao
15 Septemba 2007Matangazo
Aliekuwa waziri mkuu wa Pakistan bibi Benazir Bhutto amesema anatarajia kurejea nchini mwezi ujao baada ya kujiweka mwenyewe katika hifadhi ya kisiasa nje ya nchi kwa miaka kadhaa.
Bibi Bhutto ambae amekuwa anafanya mazungumzo na rais Pervez Musharraf juu ya kugawana mamlaka ya uongozi amesema anatumai kuwa watu wa Pakistan wanataka kurejeshwa demokrasia nchini na amteoa mwito kwa watu hao kuenda uwanja wa ndege na kumpokea atakaporejea tarehe 18 ya mwezi ujao.