ISLAMABAD: Polisi Pakistan wavunja maandamano
17 Machi 2007Matangazo
Maandamano yameendelea nchini Pakistan kupinga hatua ya kumfukuza kazi hakimu-mkuu Iftikar Muhammad Chaudhry.Ripoti zinasema,maandamano yamefanywa katika miji ya Karachi,Lahore na Rawalpindi.Polisi mjini Lahore,walitumia mabomu ya kutoa machozi kuwatawanya waandamanaji waliyojaribu kulivamia jengo la mahakama,wengi wao wakiwa wanasheria.Hapo awali,polisi 14 walifukuzwa kazi,kwa sababu hiyo jana,walijaribu kwa nguvu,kuzuia matangazo ya kituo cha televisheni cha binafsi,kilichokuwa kikirusha matangazo ya ghasia hizo.Chaudhry aliachishwa kazi na Rais Pervez Musharraf mwanzoni mwa mwezi huu kwa shutumu kuwa ametumia vibaya madaraka yake.