ISLAMABAD: Musharraf azuru Saudi Arabia | Habari za Ulimwengu | DW | 20.11.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

ISLAMABAD: Musharraf azuru Saudi Arabia

Rais Pervez Musharraf wa Pakistan ameondoka leo kwenda nchini Saudi Arabia kukutana na mfalme Abdullah. Hiyo ni ziara yake ya kwanza tangu alipotangaza hali ya hatari mnamo tarehe 3 mwezi huu na inafanyika siku moja baada ya mahakama kuu kumuondolea malalamiko yaliyowasilishwa kupinga kuchaguliwa kwake.

Leo tume ya uchaguzi imeidhinisha tarehe ya uchaguzi kuwa Januari 8.

Pia maafisa wa Pakistan wameanza kuwaachilia huru baadhi ya wafuasi wa upinzani waliokamatwa tangu hali ya hatari ilipotangazwa.

Wafuasi wengi walioachiliwa usiku wa kuamkia leo, ni mawakili na raia wa kawaida. Wanaharakati na viongozi mashuhuri wa upinzani kama vile mchezaji kriketi wa zamani, Imran Khan, bado wanazuililiwa gerezani.

Katika mkoa wa kusini, watu 300 wakiwemo mawakili, watetezi wa haki za binadamu na wafuasi wa kiongozi mkuu wa upinzani, Benazir Bhutto, wameachiliwa huru.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com