1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Iran yalalamika kuhusu timu yake katika Kombe la Dunia

20 Juni 2026

Katibu Mkuu wa Shirikisho la Soka la Iran Hedayat Mombeyni, amesema hatua zinazochukuliwa dhidi ya Iran katika michuano ya Kombe la Dunia ni ''aibu” kwa historia ya mashindano hayo.

https://p.dw.com/p/5Fkdq
Kombe la Dunia 2026 | michuano
Timu ya soka ya Iran katika mchuano na NewZealand mnamo Juni 15, 2026Picha: Daniel Cole/REUTERS

Mombeyni alikuwa akizungumza na waandishi wa habari katika uwanja wa mazoezi wa timu hiyo huko Tijuana Mexico, siku moja baada ya shirikisho hilo kutangaza kuwa litawasilisha malalamiko kwa shirikisho la soka ulimwenguni,  FIFA  likidai kuwa timu hiyo inawekewa vikwazo vya usafiri vinavyohatarisha uwezo wake wa kufanya vizuri kwenye mashindano hayo.

Amesema mashindano hayo ni makubwa ya kimataifa na kwamba kuvunjwa kwa kanuni na makubaliano kwa namna hiyo kwa maoni yake kunatilia mashaka hata mchezo wa soka wenyewe.

Iran  ilitaka kusafiri kwenda Marekani siku mbili kabla ya mechi yake ijayo dhidi ya Ubelgiji huko Los Angeles siku ya Jumapili, kwa sababu mchuano huo unatarajiwa kuanza saa sita mchana kwa saa za huko, lakini ombi lao kuruhusiwa kufanya hivyo lilikataliwa.

Ubelgiji ilisafiri jana Ijumaa kuelekea California siku mbili kabla ya mechi hiyo.