1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Iran yaishambulia Tel Aviv na kuwajeruhi watu sita

26 Machi 2026

Iran imeshambulia kwa makombora maeneo kadhaa ya eneo kubwa la Tel Aviv leo asubuhi. Haya yameelezwa na jeshi la Israel.

https://p.dw.com/p/5B9VG
Israel Bnei Brak 2026 | shambulizi la Iran
Uharibifu wa shambulizi la Iran mjini Tel Aviv, Israel, mnamo Machi 24, 2026Picha: Ilia Yefimovich/AFP

Jeshi hilo pamoja na huduma za dharura, pia zimeripoti kusikia kwa ving'ora katika maeneo mengi ya Israeli, ikiwa ni pamoja na miji ya Tel Aviv, Jerusalem na kaskazini mwa nchi, huku athari zikiripotiwa katika maeneo mengine kadhaa.

Wakati huo huo, Israel imelenga shabaha mpya kote Iran hii leo, baada ya Tehran kukataa mipango ya Marekani ya kumaliza vita vya Mashariki ya Kati ambavyo vimedumu sasa kwa takriban wiki nne. Iran pia imeishambulia UAE ambapo mjini Abu Dhabi mamlaka imesema watu wawili wameripotiwa kuuawa baada ya kuangukiwa na mabaki ya kombora lililodunguliwa.

Kwa upande mwingine kwenye mahojiano ya televisheni waziri wa mambo ya nje wa Iran Abbas Araghchi amesema serikali yake haijashiriki mazungumzo ya kumaliza vita, na haina mpango wa mazungumzo yoyote.