1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Iran na Marekani zafanya mazungumzo Oman

6 Februari 2026

Iran na Marekani zimeanza leo mazungumzo nchini Oman, huku Washington ikikataa kuondoa kitisho cha hatua za kijeshi dhidi ya jamhuri hiyo ya Kiislamu .

https://p.dw.com/p/58Ccl
Oman Muskat 2026 |Mazungumzo ya Iran na Marekani
Waziri wa mambo ya nje wa Oman Sayyid Badr Hamad Al Busaidi( kulia) akiwa na wajumbe wa Marekani katika mazungumzo na Iran mjini Muscat mnamo Februari 6, 2026Picha: Oman Foreign Ministry/Anadolu Agency/IMAGO

Mjumbe wa Rais wa Marekani Donald Trump Mashariki ya Kati Steve Witkoff na waziri wa mambo ya nje wa Iran Abbas Araghchi wanaongoza wajumbe wao katika mazungumzo hayo Oman, ambayo ni mpatanishi kati ya nchi hizo mbili.

Vyombo vya habari vya Iran vimeripoti kuwa mazungumzo hayo yameanza, huku Araghchi akisema Tehran inasisistiza kuhusu utayari wa kutetea uhuru na usalama wa taifa dhidi ya matakwa yoyote ya kupitiliza ya Marekani.

Iran yaingia katika diplomasia na umakini

Katika chapisho kwenye mtandao wa X, Araghchi amesemaIraninaingia katika diplomasia kwa umakini na kumbukumbu thabiti ya yaliotokea mwaka uliopita. Hata hivyo ameongeza kuwa wanashirikiana kwa nia njema na msimamo thabiti wa haki zao.

Kwa upande wake, katibu wa habari katika Ikulu ya White House Karoline Leavitt, amesema ujumbe wa Marekani unakusudia kuangazia ''uwezo sifuri wa nyuklia" kwa Iran, na akaonya kwamba Trump ana ''njia nyingi anazoweza kutumia kando na diplomasia".