1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

IOM: Idadi ya wakimbizi wa ndani Sudan yapindukia milioni 10

11 Juni 2024

Shirika la Umoja wa Mataifa lenye dhima na uhamiaji IOM limesema idadi ya wakimbizi wa ndani Sudan imevuka milioni 10 huku vita vinavyoendelea vikisababisha robo ya jumla ya watu wa taifa hilo kusalia bila ya makazi.

https://p.dw.com/p/4gt5p
Wakimbizi wa Sudan katika hospitali ya Adre
Wakimbizi wa Sudan waliokusanyika huku timu za Madaktari Wasio na Mipaka (MSF) ikiwasaidia majeruhi wa vita kutoka Darfur Magharibi, Sudan,Picha: Mohammad Ghannam/MSF/REUTERS

Msemaji wa IOM, Mohammedali Abunajela amesema zaidi ya watu milioni mbili wamelazimika kukimbilia mataifa kama Chad, Sudan Kusini na Misri, na wengine milioni 2.8 waliyakimbia makazi yao kabla ya hata ya vita hivi vya sasa. Vita hivyo vimeiharibu Sudan na kusababisha vifo vya zaidi ya watu 14,000 na kujeruhi maelfu, huku ikiwaingiza raia katika hali ya njaa kali. Mwezi uliopita, Shirika la chakula la Umoja wa Mataifa lilionya pande zinazopigana kwamba kuna hatari kubwa ya kuenea kwa njaa na vifo katika eneo kubwa la magharibi mwa Darfur na kwingineko nchini Sudan ikiwa hawataruhusu misaada ya kibinadamu.