1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
UchumiAfrika

IMF, Benki ya Dunia, zafanya mikutano barani Afrika

Tatu Karema
10 Oktoba 2023

Mkuu wa Shirika la IMF Kristalina Georgieva, ametoa wito kwa mataifa tajiri kutoa msaada zaidi kwa nchi zinazoendelea zenye madeni

https://p.dw.com/p/4XKCB
Mkuu wa Shirika la IMF Kristalina Georgieva akizungumza na DW mnamo Februari 17.02.2023
Mkuu wa Shirika la IMF Kristalina GeorgievaPicha: DW

Georgieva amesema haya Jumatatu (09.10.2023)  wakati wa ufunguzi wa mikutano ya kwanza ya shirika hilo la IMF na Benki ya Dunia inayofanyika barani Afrika baada ya miaka 50. Katika mkutano na wanachama wa mashirika ya kiraia, Georgieva amesema kufanywa tena kwa mikutano hiyo barani Afrika ni kiashiria muhimu sana.

Bara la Afrika linakabiliwa na changamoto sawa na za miaka 50 iliyopita

Georgieva ameongeza kuwa bara Afrika linakabiliana na changamoto sawa na zilizokuwa miaka 50 iliyopita, zinazojumuisha mfumuko wa bei na machafuko ya kisiasa katika maeneo mengi.

Mataifa mengi yanakabwa na mzigo wa madeni

Georgieva pia amesema kuwa nchi nyingi zinakabiliwa na mzigo wa madeni unaoweza kuzisambaratisha na akaelezea matumaini kwamba mikutano hiyo itasaidia kujenga imani kati ya mataifa.

Georgieva ameongeza kuwa shirika la IMF na Benki ya Dunia zinahitaji uwezo zaidi kuzisaidia nchi zinazohitaji msaada ikiwa ni pamoja na kutoa mikopo yenye riba sifuri kwa kiwango kikubwa.