1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Watu waliokufa kutokana na mafuriko nchini Kongo waongezeka

7 Mei 2023

Idadi ya watu waliokufa kutokana na mafuriko na maporomoko ya ardhi katika eneo la mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, imeongezeka hadi watu 203 kutoka watu 176.

https://p.dw.com/p/4R0Sa

Idadi ya watu waliokufa kutokana na mafuriko na maporomoko ya ardhi katika eneo la mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, imeongezeka hadi watu 203 kutoka watu 176 waliothibitishwa kufa mnamo siku mbili zilizopita. Thomas Bakenga, msimamizi wa eneo la Kalehe kulipo vijiji vilivyoathiriwa na maafa hayo amesema miili hiyo 203 imetolewa kwenye kifusi katika kijiji cha Bushushuwa hadi kufikia jana Jumamosi. Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres akiwa nchini Burundi alitoa salamu za rambirambi kwa wahanga wa mafuriko katika nchi za Kongo na Rwanda. Amesema hiki ni kielelezo kingine cha kasi ya mabadiliko ya hali ya hewa na athari zake mbaya. Guterres amesikitika kwamba nchi ambazo hazijachangia kwa vyovyote ongezeko la joto duniani ndizo zinakabiliwa na athari za mabadiliko ya hali ya hewa.