1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ICJ yataka Israel kuruhusu misaada zaidi kuingia Gaza

Amina Mjahid
29 Machi 2024

Mahakama ya Kimataifa ya Haki ICJ imeiamuru Israel kuhakikisha chakula zaidi na msaada wa dharura wa kiutu vinafikishwa katika Ukanda wa Gaza, na kuonya kuwa baa la njaa linakaribia kulikumba eneo hilo

https://p.dw.com/p/4eFbV
Mahakama ya Kimataifa ya Haki ICJ
ICJ yaiamuru Israel kuhakikisha chakula zaidi na msaada wa dharura wa kiutu vinafikishwa katika Ukanda wa Gaza Picha: Piroschka van de Wouw/REUTERS

Agizo hilo la ICJ limekuja baada ya Umoja wa Mataifa kusema mara kadhaa kwamba eneo lililozingirwa la Gaza huenda likakumbwa na Baa la njaa baada ya Israel kukataa chakula kuingizwa huko. 

Mashambulizi yaendelea kurindima Gaza

Hayo yanajiri wakati mzozo wa takriban miezi sita kati ya Israel na kundi la wanamgambo wa Hamas ukiendelea na wizara ya Afya Gaza, ikisema hadi sasa watu 32,623 wameuawa katika mzozo huo huku zaidi ya watu 75,000 wakijeruhiwa.