Sheria na HakiSudan
ICC yamkuta na hatia Mkuu wa wanamgambo Janjaweed wa Sudan
6 Oktoba 2025
Matangazo
Ali Muhammad Ali Abd-Al-Rahman, anayejulikana pia kama Ali Kushayb , alipatikana na hatia ya makosa mengi ya uhalifu ikiwa ni pamoja na ubakaji, mauaji na mateso yaliyotekelezwa kati ya Agosti 2003 na Aprili 2004 vilivyofanywa wakati wa mashambulizi ya kikatili huko Darfur , lakini mwenyewe alikana mashtaka hayo.
Joanna Korner, Jaji kiongozi wa ICC yenye makao yake mjini The Hague Uholanzi amesema mahakama hiyo inao ushahidi wa kutosha kuwa mshtakiwa aliyekuwa mkuu wa wanamgambo wa Janjaweed huko nchini Sudan ana hatia kwa makosa yanayomkabili huku akisisitiza kuwa hukumu ya adhabu yake itatolewa hapo baadaye.