1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JamiiSomalia

HRW yaitaka Somalia kutobadili sheria ya haki za watoto

29 Machi 2024

Shirika la Human Rights Watch limeitaka Somalia kutupupilia mbali marekebisho ya katiba ambayo yanalenga kupunguza umri wa utu uzima kisheria, likidai kwamba mageuzi hayo yatadhoofisha haki za watoto.

https://p.dw.com/p/4eG8u
 HRW yadai kwamba mageuzi hayo yatadhoofisha haki za watoto nchini Somalia
HRW yadai kwamba mageuzi hayo yatadhoofisha haki za watoto nchini SomaliaPicha: John MacDougall/AFP/Getty Images

Shirika la kimataifa la kutetea haki za binaadamu la Human Rights Watch limeitaka Somalia kutupupilia mbali marekebisho ya katiba ambayo yanalenga kupunguza umri wa utu uzima kisheria, likidai kwamba mageuzi hayo yatadhoofisha haki za watoto.

Mabadiliko yaliyopendekezwa na ambayo yatajadiliwa bungeni Jumamosi yanatofautisha kati ya umri wa utu uzima wa miaka 15 na miaka 18 kama umri wa kuwajibika kisheria.

Aidha, shirika hilo la kutetea haki za binadamu limesema sheria hiyo itazua utata katika utekelezaji wake nchini Somalia. Human Rights Watch imesema mabadiliko yaliyopendekezwa yatawaweka wasichana katika hatari kubwa ya ndoa za utotoni, ambayo huathiri afya zao, haswa afya ya uzazi, upatikanaji wa elimu, na ulinzi wao dhidi ya aina zingine za unyanyasaji.

Kulingana na shirika la kimataifa la Girls Not Brides, asilimia 26 ya wasichana nchini Somalia huolewa kabla ya umri wa miaka 18, na asilimia 17 kabla ya umri wa miaka 15.