Hillary Clinton kutoa ushahidi sakata la Epstein
17 Februari 2026
Aliyewahi kuwa waziri wa mambo ya nje nchini Marekani Hillary Clinton ameonesha kutilia mkazo msimamo wake kuhusu sakata la mtuhumiwa wa unyanyasaji wa kingono, Jefrey Epstein, akidai watu wote waliotakiwa kutoa ushahidi , akiwemo Andrew, mwanawe hayati malkia Elizabeth wa pili wa Uingereza, wanapaswa kufika mbele ya kamati ya bunge inayochunguza kadhia hiyo.Mshirika wa Epstein Maxwell aomba msamaha kwa Trump kabla ya kutoa ushahidi
Clinton ambaye pia ni mkewe rais wa zamani Bill Clinton anatarajiwa kufika mbele ya kamati hiyo tarehe 26 mwezi huu kutowa ushahidi wake, siku moja kabla ya mumewe.
Clinton amekuwa akiishinikiza serikali ya rais Donald Trump kuchapisha nyaraka zote zilizobakia kuhusu sakati la Epstein.
Wote wawili wametaka kikao cha kusikilizwa ushahidi wao kifanyike hadharani badala ya faragha.