Heiko Maas apinga vikwazo zaidi kwa Urusi | Matukio ya Kisiasa | DW | 26.04.2021
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Matukio ya Kisiasa

Heiko Maas apinga vikwazo zaidi kwa Urusi

Waziri wa mambo ya kigeni wa Ujerumani, Heiko Maas amekataa miito ya vizuizi vikali zaid dhidi ya Urusi, kutokana na namna inavyomtendea Alexei Navalny pamoja na kujiimarisha kijeshi kwenye mpaka wa Ukraine.

Akizungumza na kituo cha utangazaji cha Ujerumani cha ARD, Maas ameuelezea uhusiano uliopo sasa kati ya Ujerumani na Urusi kuwa ni mbaya kabisa, lakini akisema hautakiwi kuendelea kuwa hivyo.

Amesema serikali ya Ujerumani inatakiwa kujihusisha zaidi na majadiliano na Urusi na kuongeza kuwa hicho ni kiini cha demokrasia.

soma zaidi: Zelensky, Macron, Merkel wazungumzia Ukraine mashariki

Katika hatua nyingine Maas amesema vikwazo vya Ujerumani dhidi ya Urusi kufuatia hatua yake ya kuinyakua Rasi ya Crimea vitaendelea hadi pale kutakapopatikana suluhu ya kisiasa.

Wakati huo huo, mahakama moja mjini Moscow imeyapiga marufuku mashirika yanayoongozwa na Navalny kuendesha shughuli zake.