Hatari ya kuzuka ghasia Burundi | Matukio ya Kisiasa | DW | 10.07.2015
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Matukio ya Kisiasa

Hatari ya kuzuka ghasia Burundi

Umoja wa Mataifa umesema Burundi ipo katika hatari ya kutumbukia katika machafuko, huku generali aliyehusika na jaribio la mapinduzi, Leonard Ngendakumana, akisema juhudi bado zinaendelea kumuondoa madarakani Nkurunziza.

Mkuu wa tume ya kutetea haki za binaadamu ya Umoja wa Mataifa, Zeid al-Hussein, ameonya leo kuwa kuna hatari ya kuripuka kwa mchafuko nchini Burundi. Hatari ambayo inatokana na rais Pierre Nkurunziza kugombea muhula wa tatu. Pamoja na hatua kali zinazochukuliwa na vikosi vya usalama, ambavyo pia vinasaidiwa na kundi la vijana wanaoitwa Imbonerakure ambalo ni tawi la chama tawala linalosemekana kuhusika na vifo kadhaa vya hivi karibuni.

"Hatari dhidi ya vifo vya binadamu, usalama wa kikanda na maendeleo ipo juu nchini Burundi. Mgogoro unaotokana na uamuzi wa rais Pierre Nkurunziza ya kugombea awamu ya tatu, umedhoofisha muongo mzima wa maendeleo ya kasi katika ujenzi wa taasisi za kidemokrasia, na mafanikio ya ujenzi wa jamii iliyoshikamana," amesema Zeid Raad al-Hussein

al-Hussein amesema ofisi yake inakumbukumbu zinazothibitisha mauwaji ya wandamanaji kadhaa pamoja na watetezi wa haki za binadamu, yaliyofanywa na vikosi vya uslama pamoja na vijana wa kundi la Imbonerakure.

Amisistiza seriklai ya Burundi iwapokonye silaha vijana wa kundi hilo, ambalo ni tawi la chama tawala cha CNDD-FDD.

Upinzani wapinga Nkurunziza kuwania awamu ya tatu

Prinz Zeid al-Hussein

Mkuu wa tume ya kutetea haki za binaadamu wa Umoja wa Matifa Zeid al-Hussein

Wakati huo huo Genarali Leonard Ngendakumana ambae ni mmoja wa waliohusika na jaribio la mapinduzi dhidi ya rais Nkurunziza mwezi Mei, amesema kundi lake bado linaendelea na jitihada za kumuondoa madarakani raisi huyo. Pia amemshutumu Nkurunziza kuchochea uhasama baina ya makabila ya wahutu na watutsi katika nchi mabayo iligubikwa na vita vya wenyewe kwa wenyewe.

Hata hivyo serikali inakana shutuma hizo kuwa kugombea muhula wa tatu kwa Nkuzunziza kutaigawanya nchi hiyo kimakabila, badala yake inasema hizo ni njama za upinzani za kuzusha ghasia kwa kuhofia kushindwa katika uchaguzi wa urais unaotarajiwa kufanyika wiki ijayo.

Burundi inakabiliana na vurugu tangu mwezi Aprili baada ya tangazo la azma ya rais Nkurunziza la kugombea muhula wa tatu. Waandamanaji wanasema rais huyo lazima aondoke madarakani kutona na kuwa katiba inaruhusu awamu mbili tu za miaka mitano. Lakini wafuasi wa rais huyo wanasema Nkurunziza anastahili awamu ya tatu ya urais kwani mara ya kwanza alichaguliwa na bunge na sio wananchi.

Msemaji mkuu wa Umoja wa Mataifa Stephane Dujarric amesemea zaidi ya warundi 140,000 wameikimbia nchi hiyo kwa kuhofia ukatili wa kundi la vijana wa Imbonerakure. Umoja wa Mataifa umetishia kuweka vikwazo dhidi ya wale waliochochea ghasia Burundi.

Mwandishi: Yusra Buwayhid/rtre/ape

Mhariri:Mohammed Abdul-Rahman

Matangazo

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com