HARARE : Mugabe kuwania tena urais mwaka 2008 | Habari za Ulimwengu | DW | 31.03.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

HARARE : Mugabe kuwania tena urais mwaka 2008

Chama tawala nchini Zimbabwe ZANU-PF kimemchaguwa Rais Robert Mugabe kuwa mgombea wake tena katika uchaguzi wa urais uliopangwa kufanyika hapo mwakani.

Uamuzi huo umefikiwa katika mkutano wa kamati kuu ya chama cha ZANU-PF katika mji mkuu wa Harare.Chama cha upinzani cha MDC imeuita uamuzi huo kuwa wa kusikitisha kwa nchi hiyo kwa kusema kwamba Mugabe mwenye umri wa miaka 83 tayari ameitawala vibaya nchi hiyo kwa miaka 27.

Msemaji wa serikali ya Marekani pia ameuita uamuzi huo wa kumuwezesha Mugabe kuwania kipindi kengine madarakani kuwa wa kuhuzunisha na wa aibu.

Mugabe amekuwa chini ya shinikizo la kimataifa linalongezeka kufuatia kuwaandama wapinzani wake wa kisiasa kwa matumizi ya nguvu hivi karibuni.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com