HAMBURG: Mounir el -Motassadeq arudishwa jela mjini Hamburg | Habari za Ulimwengu | DW | 18.11.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

HAMBURG: Mounir el -Motassadeq arudishwa jela mjini Hamburg

Mshitakiwa wa kwanza kuhukumiwa kuhusika na mashambulizi ya Septemba 11 nchini Marekani, Mounir el Motassadeq, amewekwa jela katika mji wa Hamburg kaskazini mwa Ujerumani. Kukamatwa kwake tena kumefuatia uamuzi wa mahakama kuu ya Ujerumani wa kufutilia mbali uamuzi wa mahakama ya chini ambayo ilimuachilia huru kwa dhamana hadi atakapohukumiwa. Mounir el Motassadeq, raia wa Morroco, mwanafunzi nchini Ujerumani, amepatikana na hatia ya kusaidia katika mauaji ya abiria 246 wa ndege zilizotumiwa na magaidi katika mashambulizi ya kujitoa mhanga kwenye miji ya New York na Washington. Motassadeq ambae aliachiliwa huru mwezi Februari mwaka huu, huenda akafungwa miaka 15 jela. Hiyo ndiyo adhabu iliokuwa imetolewa katika kesi ya kwanza kwa hatia ya kuhusika na mauaji ya watu zaidi ya 3,000 na kushiriki katika kundi la kigaidi.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com