1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Hali tete Pakistan

9 Septemba 2007
https://p.dw.com/p/CBRe

Maafisa nchini Pakistan wamefahamisha kuwa kitisho cha mashambulio ya kigaidi kinaweza kutokea na kutokana na hali hiyo maafisa wamewekwa katika hali ya kuwa tayari kukabiliana na chochote katika viwanja vya ndege nchini humo.

Serikali pia imepiga marufuku mikusanyiko ya watu watano au zaidi karibu na uwanja wa ndege wa kimataifa wa Rawalpindi.Hatua hii imekuja wakati ambapo waziri mkuu wa zamani wa nchi hiyo Nawaz Sharif anatarajiwa kurudi Pakistan kumkabili rais Pervez Musharraf katika uchaguzi licha ya kutolewa wito na Saudi Arabia asichukue hatua hiyo ya kurudi Pakistan.