Hali ni tete nchini Iran | Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili | DW | 16.06.2009
 1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Timu Yetu

Hali ni tete nchini Iran

Baraza la walinzi lapanga kuhesabu upya kura

Mdajala wa kabla ya uchaguzi kati ya wagombea wawili wakuu:Ahmedinedjad na Moussavi

Mdajala wa kabla ya uchaguzi kati ya wagombea wawili wakuu:Ahmedinedjad na Moussavi


Hali ni tete kabisa mjini Teheran ambako maandamano mawili yanasubiriwa hii leo katika uwanja mmoja na kupishana kwa muda mfupi tuu;ya kwanza ya wafuasi wa rais Mahmoud Ahmedinedjad na ya pili ni ya wale wanaopinga kuchaguliwa kwake.Baraza la walinzi limekiri kura zihesabiwe upya.

Baraza la walinzi limesema hii leo liko tayari kuanza upya kuhesabu kura za uchaguzi wa rais wa June 12 iliyopita.Kwa mujibu wa kituo cha televisheni cha Press TV,taasisi hiyo ya bunge imejulisha huenda zoezi hilo la kuhesabiwa upya kura likapelekea kutangazwa matokeo mepya kuwahusu wagombea wawili wakuu.

Mpenda mageuzi,Mir Hussein Mossavi,anaetajikana kushindwa moja kwa moja na rais Mahmoud Ahmedinedjad,alilitaka baraza la walinzi libatilishe matokeo ya uchaguzi.

Kwa mujibu wa matokeo rasmi,mhafidhina aliyekomaa Ahmadinedjad amejikingia asili mia 63 dhidi ya asili mia 34 za kura za mpinzani wake anaefuata msimamo wa wastani.

Hata wadadisi wa masuala ya kisiasa nchini Iran wanashuku matokeo hayo.Ahmad Zeidabadi anasema:

"Matokeo yaliyotangazwa hayaambatani hata kidogo na kile tulichokishuhudia vituoni.Utaratibu mzima umeandaliwa na matokeo kutungwa tangu awali-hayalingani hata kidogo na ukweli wa mambo."

Matokeo hayo ndiyo yaliyowakera wafuasi wa Mir Hossein Moussavi,walioteremka kwa malaki jana katika eneo la kati la mji mkuu,licha ya marufuku.Na leo mchana pia wanapanga kuteremka katika uwanja ule ule wa Vali Asr,kati kati ya mji mkuu Teheran.

Iran Wahlen 2009 Gewaltsame Ausschreitungen

Waandamanaji mjini Teheran

Watu sabaa wameuwawa katika maandamano ya jana,baada ya kuzuka mapambano pamoja na kikosi kimoja cha wanajeshi.

Wazriri mkuu wa zamani Mir Husein Moussavi, anaebisha ushindi wa Ahmedinedjad ,hafikirii kushiriki katika maandamano ya leo,hata hivyo amewatolea mwito wafuasi wake,"wasinase kama alivyosema tunanukuu:" katika mtego wa mashambulio ya majiani na wasalie watulivu" mwisho wa kumnukuu.

Wafuasi wa rais Ahmedinedjad wamepanga kwa upande wao pia kukusanyika saa mbili kabla-yaani saa sita na nusu kwa saa za Afrika mashariki katika uwanja huo huo wa Vali Asr,ili kulalamika dhidi ya "machafuko na kuharibiwa mali ya umma."

Mwito wa maandamano umetolewa pia na Ayatollah mkubwa,mpinzani Hossein Ali Montazeri.Amewataka hasa vijana wa Iran waendelee na maandamano yao kudai kile alichokiita "haki zao."

Ayatollah mkubwa,aliyewahi wakati mmoja kufikiriwa kushika wadhifa wa muasisi wa jamhuri ya kiiislam ,Ayatollah Rouhollah Khomeiny,aliwahi kwa muda mrefu kutumikia kifungo cha nyumbani kutokana na lawama zake dhidi ya utawala wa Iran.

Mwandishi:Hamidou Oummilkheir/AFP

Mhariri:Abdul Rahman

 • Tarehe 16.06.2009
 • Mwandishi Oumilkher Hamidou
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/IAaM
 • Tarehe 16.06.2009
 • Mwandishi Oumilkher Hamidou
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/IAaM
Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com