1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Habari zinapingana kuhusu kuuliwa watu 26 mjini Baghdad

30 Juni 2007
https://p.dw.com/p/CBn4

Baghdad:

Uongozi wa kijeshi wa Marekani umetangaza kuwauwa wafuasi 26 wa itikadi kali katika mashambulio ya alfajiri ya leo mjini Baghdad.Lakini wakaazi wa mji mkuu huo wa Irak wanasema wote waliouliwa ni raia wa kawaida.Mashambulio yalidumu saa sita,mashahidi wamesema.Uongozi wa kijeshi wa Marekani unawashikilia watuhumiwa wengine 17.Wanatuhumiwa kuingiza miripuko kutoka Iran,inayotegwa majiani.Iran imekanusha madai hayo.Shambulio la barabarani,liligharimu maisha ya wanajeshi watano wa kimarekani alkhamisi iliyopita katika mtaa wa Rasheeda kusini mwa Baghdad.Wakati huo huo viongozi wa kijeshi wa Marekani nchini Irak wamevikosoa vyombo vya habari vya kimataifa kwa kuchapisha ripoti za uongo kuhusu miili ya watu 20 waliogunduliwa wamekatwa vichwa kusini mwa Baghdad,mapema wiki hii.”Wapinzani wa vikosi vya Irak” wamesambaza habari hizo za uongo” jeshi la Marekani limesema.