GAZA:Wapalestina wauwawa Gaza | Habari za Ulimwengu | DW | 28.04.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

GAZA:Wapalestina wauwawa Gaza

Wanajeshi wa Israel wamewauwa wapalestina watatu na kumjeruhi mmoja katika ukanda wa Gaza.

Duru za Palestina zinaarifu mashambulio ya risasi yamefanyika mapema hii leo asubuhi kaskazinimagharibi mwa mji wa Gaza na karibu na eneo la usalama.

Mwanajeshi wa Israel amethibitisha shambulio hilo na kusema wapalaestina hao walikuwa wakijaribu kuweka mabomu katika eneo hilo kati ya Gaza na Israel.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com