1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Gavana akamatwa kwa ufisadi Kenya

Daniel Gakuba
4 Julai 2018

Idara ya Kupambana na Ufisadi imemtia nguvuni Gavana wa Kaunti ya Busia katika operesheni dhidi ya ufisadi ambayo kwa muda wa miezi miwili tayari imefanya misako kadhaa na kuanzisha uchunguzi kwa visa vya rushwa Kenya.

https://p.dw.com/p/30pL3
Kenja Proteste gegen Korruption an Unabhängigkeitstag
Picha: picture alliance/dpa/D. Kurokawa

Gavana huyo, Sospeter Ojaamong, hakusema mengi kuhusu tuhuma taarifa hizo, lakini alikieleza kituo cha habari cha KTN nchini Kenya kwamba yeye ni mweupe kama pamba au theluji.

Mkuu wa kitengo cha uendesha mashtaka wa umma Noordin Haji amethibitisha kwamba maafisa 9 watasimamishwa kizimbani kuhusiana na wizi wa mamilioni ya fedha za umma.

Alisema mashitaka dhidi ya Gavana Ojaamong yatajumuisha matumizi mabaya ya ofisi yake, na hila ya kuiba mali ya umma.

Tuhuma za ufisadi dhidi ya gavana huyo zinatokana na zabuni katika mfumo wa ukusanyaji taka katika mji wa Busia ulio karibu na mpaka baina ya Kenya na Uganda.