1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ethiopia yakabiliwa na hatari ya kukosa chakula cha msaada

10 Oktoba 2025

Shirika la Mpango wa Chakula Duniani WFP, limesema, linakabiliwa na hatari ya kusitisha msaada wa chakula kwa mamilioni ya wakimbizi nchini Ethiopia kutokana na kupunguzwa kwa misaada ya kimataifa.

https://p.dw.com/p/51nzM
Sudan, Port Sudan 2024 | WFP-wafanyakazi wa msaada
Malori yaliobeba msaada wa WFP kutoka Port SudanPicha: Abubakar Garelnabei/WFP/Handout/REUTERS

Mkurugenzi wa shirika hilo la WFP nchini Ethiopia, Zlatan Milisic, amesema linahitaji kukusanya takriban dola milioni 230 kuendeleza shughuli za kibinadamu kwa muda wa miezi sita ijayo.

Katika taarifa, Milisic amesema kuwa bila ya ufadhili mpya wa haraka, WFP inaweza kulazimika kusitisha kabisa msaada wa chakula kwa wakimbizi wote nchini Ethiopia katika miezi ijayo.

WFP yalazimika kupunguza mgao wa chakula

Mwezi huu, WFP ililazimika kupunguza mgao wa chakula kwa wakimbizi 780,000 katika kambi 27 kote Ethiopia.

Milisic amesema wanafanya maamuzi yasiowezekana.

Ameongeza kuwa mapunguzo hayo ni hatua nyingine ya kuelekea kusimamisha kabisa usambazaji wa chakula na kuweka maisha ya wale wanaopata msaada kwa sasa kuwa katika hali ya hatari.