Ehud Barak kuzuru Misri | Habari za Ulimwengu | DW | 23.12.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Habari za Ulimwengu

Ehud Barak kuzuru Misri

---

JERUSELEM:

Waziri wa ulinzi wa Israel Ehud Barak atafunga safari ya Misri jumatano ijayo kukutana na rais Honi Mubarak wa Misri.Ziara hii itafanyika huku chama cha HAMAS chenye kudhibiti malaka mwambao wa gaza kikisema kitayari kusimamisha mapigano na Israel ,ikiwa Israel nayo itakomesha kampeni yake ya kijeshi na kuwashambulia wanasiasa wake wenye siasa kali.

Maafisa wa Israel hawakusema kwamba wakati wa ziara yake Bw.Barak atazungumzia juhudi za kuachiwa huru Coplo Gilad Shalit, mwanajeshi wa Israel alienyakuliwa na wanamgambo wenye mafungamano na Hamas hapo juni,mwaka jana .

Taarifa nyengine kutoka Jeruselem zasema kwamba, Israel inapanga kujenga maskani zaidi za wayahudi 740 katika eneo linalogombaniwa la Jeruselem mashariki na Ukingo wa magharibi mwaka ujao.Taarifa hiyo ilitolewa leo na waziri wa Israel.Hii ni hatua ambayo bila shaka itawaudhi wapalestina wanaodai kwamba ujenzi wa maskani zaidi katika ardhi zao unachafua juhudi za kufikia amani na Israel.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com