Droo ya hatua ya 16 yafanywa | Michezo | DW | 12.12.2016
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Michezo

Droo ya hatua ya 16 yafanywa

Mabingwa wa Ulaya Real Madrid watashuka dimbani dhidi ya Napoli katika hatua ya 16 ya ligi ya Mabingwa Ulaya

Baada ya kujikatia tikiti ya kucheza katika hatua ya mwondowano, hatimaye timu zimeweza kupangwa na wapinzani wao kwa ajili ya michuano hiyo ya mikondo miwili. 

Droo kamili

Real Madrid vs Napoli
Bayern Munich vs Arsenal
PSG vs Barcelona
Sevilla vs Leicester
Benfica vs Borussia Dortmund
Porto vs Juventus 
Bayer Leverkusen vs Atletico Madrid
Manchester City vs Monaco

Michuano ya mkondo wa kwanza ya hatua ya 16 itachezwa Februari 14/15 na Februari 21/22, wakati mechi za marudiano zitachezwa Machi 7/8 na 14/15.

Robo fainali zitachdzwa Aprili 11/12 na 18/19, wakati nusu fainali zitachezwa Mei 2/3 na 9/10. Fainali itakuwa Juni 3 mjini Cardiff, Wales.

Mwandishi: Bruce Amani/DPA/AFP
Mhariri: Yusuf Saumu