DRC yapata makubaliano ya kisiasa - Upinzani | Matukio ya Afrika | DW | 23.12.2016
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

DRC

DRC yapata makubaliano ya kisiasa - Upinzani

Wanasiasa katika Jamhuri ya Kidemokarsia ya Kongo wamefikia makubaliano ya kuumaliza mkwamo wa kisiasa uliotishia kuiingiza tena nchi hiyo kwenye machafuko, baada ya muda wa Rais Joseph Kabila kumalizika kikatiba.

Kwa mujibu wa rasimu ya makubaliano hayo, ambayo shirika la habari la Reuters limepata nakala yake, sasa Rais Kabila ataondoka madarakani mwishoni mwa mwaka 2017, hatua ambayo haikutarajiwa, hasa baada ya watu zaidi ya 20 kuuawa kwenye maandamano dhidi ya Kabila wiki hii.

Wanasiasa wa upinzani waliozungumza na Reuters wanasema makubaliano hayo "yanamzuia pia Kabila kufanya mabadiliko ya katiba ambayo yangelimruhusu kuwania muhula wa tatu".

Vile vile, pataundwa serikali ya mpito ambayo itasimamiwa na waziri mkuu kutoka kundi la wapinzani lenye nguvu, huku kiongozi mkuu wa upinzani, Etienne Tshisekedi, akipewa jukumu la kusimamia utekelezaji wa makubaliano hayo.

Msemaji wa serikali amekataa kutungumzia chochote kuhusiana na makubaliano hayo, yaliyofikiwa leo chini ya usimamizi wa Kanisa Katoliki nchini Kongo.