1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroPoland

Donald Tusk:Ulaya imeingia katika "nyakati za kabla ya vita"

30 Machi 2024

Waziri Mkuu wa Poland Donald Tusk ameonya kwamba bara la Ulaya lipo katika nyakati za kabla ya vita kufuatia uvamizi wa Urusi nchini Ukraine.

https://p.dw.com/p/4eGVK
Poland | Waziri Mkuu Donald Tusk
Waziri Mkuu wa Poland Donald TuskPicha: Kuba Atys/Agencja Wyborcza.pl via REUTERS

Tusk ameyasema hayo alipokuwa akihojiwa na muungano wa magazeti manane ya Ulaya maarufu kama Lena.

Kiongozi huuyo wa Poland amesisitiza kuwa hana nia ya kumtisha yoyote, bali anaelezea hali halisi na kusisitiza kuwa chochote kinawezekana na kwamba wakaazi wote wa Ulaya wafahamu kuwa enzi mpya sasa imeanza na inabidi kuizoea hali hiyo.

Donald Tusk ameendelea kwamba ikiwa Ukraine itashindwa vita vyake dhidi ya Urusi, hakuna mtu yeyote barani Ulaya atakayeweza kujihisi kuwa salama. Hata hivyo rais wa Urusi Vladimir Putin amekuwa mara kadhaa akikanusha kuwa na nia ya kuyavamia mataifa mengine ya Ulaya.