Dira ya kitaifa ya Kenya ya 2030 imefikiwa au la? | IDHAA YA KISWAHILI | DW | 22.09.2021
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

IDHAA YA KISWAHILI

Dira ya kitaifa ya Kenya ya 2030 imefikiwa au la?

Raia nchini Kenya wana shauku ya kufahamu iwapo malengo ya mpango wa maendelo wa mwaka 2030 yatafikiwa katika wakati ufisadi na siasa za uhasama zikitajwa kama vikwazo kwa Kenya kupiga hatua. Sikiliza ripoti ya mwandishi wetu Wakio Mbogho kutoka Nakuru.

Sikiliza sauti 02:26

Ni miaka 13 tangu serikali ya Kenya ilipozindua mpango wa malengo ya mwaka 2030, kwenye azimio la kutekeleza miradi itakayoiweka Kenya kati ya mataifa yalio na uchumi wa kiwango cha katikati, kupigana na umasikini na kuwahakikishia wananchi maisha yenye ubora wa hali ya juu. Kiongozi wa chama cha upinzani, ODM Raila Odinga anaeleza.

Odinga anasema azimio hili limeonekana kuwapiga chenga viongozi serikali, akiwakosoa kwa kushamiri kwenye siasa za uhasama na ufisadi.

Aidha, viongozi wanalalamika kwamba juhudi za kuhakikisha kumekuwa na mgawanyo sawa wa rasilimali kati ya jamii zote zimekuwa zikigonga mwamba. Junet Mohammed ni mbunge wa Suna Mashariki.

Tume ya Uwiano na Utangamano nchini, NCIC, inatambua umuhimu wa wanasiasa kuuza sera zao katika kipindi hiki taifa linapojitayarisha kwa uchaguzi wa mkwa ujao, ila inaonya dhidi ya uchochezi baina ya jamii. Sam Kona, Kamishna kwenye tume hiyo anasema tayari wanaweka kumbukumbu ya matamshi na tabia za wanasiasa na watakaokiuka sheria watachukuliwa hatua.

“Wanasiasa ambao huwatusi wenzao au kuvamia mikutano yao ya umma, tumeanza kuweka kumbukumbu zao na hatua mwafaka itachukuliwa. Hakuna vile taifa hili litarudia matukio ya mwaka 2007. Wakenya wakatae kugawanywa, wawambie wanasiasa wawauzie sera zao na sio kusababisha hofu kati yako na jirani yako,” amesema Kona.

Mpango wa malengo ya mwaka 2030 umejikita kufanya mageuzi katika sekta za elimu, miundo mbinu, afya, huduma za umma, usalama na utawala wa taifa.