Cologne yarejea Bundesliga | Michezo | DW | 07.05.2019
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Michezo

Cologne yarejea Bundesliga

Cologne imerejea kwenye Bundesliga baada ya ushindi wa 4-0 dhidi ya Greuther Fürth. Lakini maswali yanabaki kuhusu uwezo wa klabu hiyo kuwa imara msimu ujao.

"Huku ni kupandishwa kwa Markus Anfang," alisema kocha wa muda wa Cologne Andre Pawlak baada ya ushindi wa mabao 4-0 wa klabu hiyo uliosababisha kurejea katika ligi kuu ya kandanda ya Ujerumani, Bundesliga.

Tatizo moja tu ni kwamba Markus Anfang hakuwepo.

"Tumeifikisha msitari wa mwisho, lakini pongezi zinawaeddea wachezaji na timu ya walimu ya zamani," Pawlak aliendelea kusema.

Timu ya zamani ya wakufunzi, iliyoongozwa na Anfang, ilitimuliwa wiki moja kabla baada ya kucheza mechi nne bila ushindi na kuifanya klabu kushindwa kupanda daraja mapema kuliko ilivyotarajiwa.

Nyuma ya furaha ya kujiunga tena na Ligu kuu ya Bundesliga, matatizo yalianza kujitokeza kwenye klabu ya Cologne and kipindi hiki cha mwisho wa msimu kitadhihirisha mipango ya klabu hiyo kuimarisha nafasi yake kama klabu ya daraja la juu.

Kiini cha matatizo ni Meneja Mkuu Armin Veh, ambaye anatakiwa kutoa matokeo katika muda wa miezi mitatu ijayo iwapo Cologne inataka mafanikio.

DFB-Pokal 2. Runde | 1. FC Köln vs. FC Schalke 04 | Trainer Markus Anfang (Getty Images/Bongarts/L. Baron)

Markus Anfang, kocha ya Cologne alietimuliwa na meneja mkuu Armin Veh.

Nyakati za mchafukoge

Veh amekuwa mashuhuri katika kipindi cha miezi 18 alichokaa Cologne. Meneja huyo mweye umri wa miaka 58 alishirika katika mapambano ya ndani ya madaraka mwezi Machi, ambayo yalisabisha kujiuzulu kwa rais wa klabu Werner Spinner, na kuimarisha mamlaka yake kwa kumfuta kazi kikatili Anfang mwishoni mwa mwezi Aprili.

Udhaifu katika safu ya ulinzi ya timu - ikiwa imefungwa magoli 41 katika mechi 31 - haukustahili kwa kinara wa ligi na mazingira duni ya chumba cha kubadilishia nguo yaliripotiwa kuwa kilele cha mambo.

"Licha ya nafasi nzuri ya kuanzia, kulikuwepo na mwekeleo hasi," Veh alisema. "Ilikuwa ni muhimu kubadili mambo kuepusha kuyaweka hatarini malengo yetu."

Mbinu hizo za kuongeza ushawishi zimeiacha klabu hiyo bila rais - mrithi wa Spinner atachaguliwa wakati uchaguzi wa bodi mwezi Septemba - na bila kocha. Hili si jambo jema kwa klabu inayotaka kuingia tena Bundesliga.

Teuzi mbili za mwisho za Veh - Anfang na Stefan Ruthenbeck - hazijafanya kazi ipasavyo. Hatua moja nyingine ya makosa na mustakabali wa Veh utakuwa mashakani.

1. FC Köln - Armin Veh Geschäftsführer Sport des 1. FC Köln (picture-alliance/dpa/R. Vennenbernd)

Meneja Mkuu wa FC Cologne Armin Veh, (kushoto) akizungumza katika mkutano na waandishi habari mjini Cologne, akiwa sambamba na Meneja mwenza Alexander Werle (katikati) na rais wa klabu Werner Spinner (kulia).

Shinikizo la muda

"Jambo muhimu ni kutoshinikizwa," Veh alisema. "Natumai kufanya maamuzi sahihi, lakini siyo chini ya shinikizo lolote la muda."

Bruno Labbadia, Pal Dardai, na David Wagner wote wamepigiwa chapuo kama warithi watarajiwa, ingawa wote wameripotiwa kuondolewa uwezekano kwa njia moja au nyigine. Achim Beierlorzer wa klabu ya Regensburg ametajwa kuwa chaguo zuri baada ya kuvutia katika nafasi yake ya kwanza ya ukocha katika daraja la pili.

Lakini wa karibuni zaidi kutajwa ni Dieter Hecking. Sio chaguo jema kwa mashabiki wenye shauku ya soka nzuri. Lakini ni chaguo salama ambalo linaweza kuituliza tena klabu na amedhihirisha kuwa na rekodi nzuri akiwa Wolfsburg na karibuni zaidi Borussia Mönchengladbach.

Jambo moja la uhakika ni kwamba shinikizo liko kwa Veh, na linahusisha saa ya kupima muda, bila kujali ni kiasi gani Meneja huyo mkuu anapinga. Kocha mpya lazima awe muhimu katika kufufua kikosi na kuwaandaa kwa mikimiki ya Bundesliga, ambako kuna dharura.