Chuck Blazer akiri kupokea rushwa katika FIFA | Michezo | DW | 04.06.2015
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Michezo

Chuck Blazer akiri kupokea rushwa katika FIFA

Aliyekuwa mwanachama wa FIFA Chuck Blazer amekiri kuwa alipokea hongo. Blazer amesema yeye pamoja na wenzake walipokea rushwa ili kuipigia kura Ufaransa kuandaa Kombe la Dunia mwaka wa 1998 na Afrika Kusini 2010

Wizara ya Sheria ya Marekani imechapisha taarifa pana inayoelezea jinsi Afisa wa zamani wa kamati kuu ya FIFA Chuck Blazer alivyokiri kuwa yeye pamoja na wenzake walipokea rushwa ili kuichagua Ufaransa kuandaa Kombe la Dunia 1998 na Afrika Kusini mwaka 2010.

Taarifa hiyo imeweka wazi mtandao wa malipo ya rushwa ulivyokuwa ukifanywa ndani ya shirikisho la soka duniani FIFA, taarifa zinazoegemea uchunguzi uliofanywa na shirika la kijasusi la Marekani FBI.

Taarifa hiyo ambayo inamwelezea Afisa huyo wa zamani wa Fifa Chuck Blazer kukiri kupokea rushwa sasa huenda ikaibua mengi kwenye kashfa ya rushwa inayolindamana shirikisho la FIFA.

Mmerakani huyo alikuwa ni mmoja wa watu waliotengeneza mipango ya kupokea rushwa katika tukio jingine la fainali la kombe la dunia 1998 nchini Ufaransa.

Taarifa za Kukiri zipo katika maandishi wakati kesi yake ilipokuwa akisikilizwa katika mahakama ya Easten New York Marekani mwaka 2013 huko ambapo alikiri makosa kumi yaliyokuwa yanamkabili.

Blazer alikuwa afisa wa ngazi juu wa FIFA eneo la kanda ya Amerika Kaskazini, Kati na Ukanda wa nchi za Karibea kuanzia mwaka 1990 hadi mwaka 2011.

Marekani imefungua kesi ya rushwa inayowakabili maafisa wa FIFA jambo lililofanya Rais wa FIFA Sepp Blatter kuamua kutangaza kujiuzulu.

Mwendesha mashtaka wa Marekani wiki iliyopita aliwashtaki maafisa 14 wa ngazi wa juu wa FIFA kwa madai ya rushwa na ulaghai

Mwandishi: Bruce Amani/AFP
Mhariri: Charo Josephat