China yatoa dola bilioni 60 kwa maendeleo Afrika | Matukio ya Afrika | DW | 04.12.2015
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Matukio ya Afrika

China yatoa dola bilioni 60 kwa maendeleo Afrika

Rais wa China Xi Jinping amewaambia viongozi wa Afrika, nchi yake itatoa dola bilioni 60 kufadhili miradi ya maendeleo barani Afrika. Xi ameyasema hayo katika mkutano wa kilele wa ushirikiano kati ya China na Afrika.

Xi, anayeuongoza mkutano huo ameorodhesha mpango wa maendeleo wa maendeleo wenye vipengee kumi wa taifa lake barani Afrika akisema anataka kujenga uhusiano wa haki na washirika walio sawa.

"Katika kuhakikisha utekelezwaji wa hatua hizi 10 za ushirikiano, China imeamua kutoa dola bilioni 60 ya kuendeleza miradi hiyo," alisema Xi katika mkutano huo unaofanyika mjini Johannesburn Afrika Kusini.

Hatua hizi zinanuiwa kuangazia mambo matatu yanayoaminika kuirejesha Afrika nyuma kimaendeleo, ambayo ni masuala ya, miundo mbinu, ukosefu wa wataalamu walio na ujuzi mbali mbali na ukosefu wa fedha za kuendeleza miradi hiyo.

Rais wa China Xi Jinping, rais wa Afrika Kusini Jacob zuma

Rais wa China Xi Jinping, rais wa Afrika Kusini Jacob zuma

Xi Jinping ameongeza kwamba fedha zitakazotolewa zitajumuisha dola bilioni tano ya mikopo isiyokuwa na riba na dola bilioni 35 ya mikopo ilio na mashrti nafuu itakayotolewa kwa Afrika. Katika hotuba yake ya ufunguzi kwenye mkutano huo, Xi pia alitangaza msaada wa kupambana na ukame barani Afrika.

"China ina wasiwasi mkubwa juu ya mavuno duni yaliosababishwa na mvua ya El Nino katika mataifa mengi ya Afrika na itatoa dola milioni 156 ya kushughulikia msaada wa vyakula vya dharura katika maeneo yatakayoathirika," alisema Xi Jinping.

China kuwekeza zaidi barani Afrika

Kando na uchumi wa china kupungua au kukuwa kwa kasi ndogo, na kusababisha Beijing kukatiza uwekezaji wake Afrika kwa zaidi ya asilimia 40 katika miezi sita ya mwanzo ya mwaka huu wa 2015, Xi amesema china itaimarisha hatua za uwekezaji katika viwanda vinavyotengeneza chakula kwaajili ya soko la nje, pamoja na kujenga barabara, bandari na reli, katika bara la Afrika linaloonekana kuwa na soko kubwa kutoka China.

Rais huyo wa China amesema nchi yake pia itaimarisha ushirikiano wake barani Afrika katika vita vyake dhidi ya makundi yalio na itikadi kali na imesema haitoingilia michakato ya kiasiasa ya serikali za bara hilo.

Baahi ya maendeleo yanayofanywa na China barani Afrika

Baahi ya maendeleo yanayofanywa na China barani Afrika

Afrika kwa ujumla inaiona China kama mpambanaji mzuri kuliko ushawishi wa Magharibi, japokuwa mataifa hayo ya Magharibi yanaishutumu China kwa kufumbia macho migogoro na ukiukwaji wa haki za binaadamu unaofanyika barani Afrika wakati wanapojiingiza barani humo kibiashara.

Mkutano huo wa siku mbili wa ushirikiano kati ya China na Afrika ni wa pili kufanyika ambapo China inawakusanya pamoja viongozi wa Afrika tangu kuzinduliwa kwake mjini Beijing mwaka wa 2000.

Tangu wakati huo biashara ya China Barani Afrika imeipiku ile ya washirika wake wa Ulaya na Marekani

Mwandishi: Amina Abubakar/ Reuters, AFP,

Mhariri: Josephat Charo